Milioni 120 gharama ya kujifunza urubani Tanzania

Taasis ya Taifa ya Usafirishaji (NIT) imetangaza kuwa mafunzo ya urubani nchini Tanzania yatagharimu Shilingi milioni 120, hatua inayopunguza kwa kiasi kikubwa mzigo wa kifedha ikilinganishwa na kusoma nje ya nchi, ambako gharama zinakadiriwa kuwa kati ya Shilingi milioni 200 na milioni 300.

Akizungumza jijini Dodoma Alhamisi, Machi 20, 2025, wakati wa kuwasilisha mafanikio ya serikali ya awamu ya sita, Mkuu wa NIT, Prof. Zacharia Mganilwa, alisisitiza kuwa kuanzishwa kwa mafunzo ya urubani ndani ya nchi kutarahisisha upatikanaji wa elimu ya anga kwa Watanzania.

“Tumekuwa tukipeleka wakufunzi wa urubani nje ya nchi kwa gharama ya Shilingi milioni 300 kwa kila mmoja. Hata hivyo, kwa kuanzisha mafunzo haya hapa nchini, tunalenga kupunguza gharama na kufanya elimu ya urubani ipatikane kwa urahisi zaidi,” alisema Prof. Mganilwa.

Aidha, alibainisha kuwa NIT ipo kwenye mazungumzo na taasisi mbalimbali ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na msaada wa kifedha kwa wanafunzi wanaotamani kuwa marubani lakini wanakumbwa na changamoto za kifedha.

Mbali na mafunzo ya urubani, NIT pia inatoa Shahada ya Uhandisi wa Matengenezo ya Ndege, ambayo hugharimu Shilingi milioni 6 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka minne, na kufanya jumla ya gharama kufikia Shilingi milioni 24.

Prof. Mganilwa aliwataka Watanzania kuchangamkia fursa hii, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kukuza utaalamu wa ndani katika sekta ya anga.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *