Salum Mayanga kocha mpya kikosi cha Mashujaa fc

Kocha mkongwe wa soka nchini, Salum Mayanga, amefikia makubaliano ya kuwa kocha mkuu wa klabu ya Mashujaa FC, akichukua nafasi ya Mohammed Bares katika mabadiliko mapya ya benchi la ufundi ndani ya klabu hiyo.

Salum Mayanga msimu huu akiwa na Mbeya City ameingia robo fainali ya Kombe la shirikisho la CRDB па pia yupo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Championship akiwa na alama 49.

Mayanga, anayefahamika kwa uzoefu wake mkubwa kwenye soka la Tanzania, aliwahi kuiongoza timu ya taifa (Taifa Stars) mwaka 2017.

Safari yake mpya inampeleka Kigoma, ambako ataanza rasmi majukumu yake Jumatano, Machi 19, 2025, baada ya kuondoka Mbeya City kuungana na kikosi chake kipya.

Mashujaa FC, kwa upande wao, tayari wamewasili Kigoma kwa mazoezi maalum baada ya kukamilisha maandalizi yao jijini Dar es Salaam.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *