Beki wa Yanga aongezwa cheo jeshini

Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo

Zanzibar (KMKM), kimempandisha cheo nyota wa timu ya Yanga SC, Ibrahim Hamad “Ibra Bacca” kutoka Koplo na kuwa Sajenti kutokana na kuonesha kiwango bora kwenye mchezo wa soka.

Mkuu wa KMKM, Azana Msingiri, amenukuliwa akisema amefikia uamuzi wa kumpandisha cheo Sajini Ibrahim kwa uwezo mkubwa aliouonyesha katika eneo la mpira wa miguu klabuni na katika timu za taifa.

Akizungumza baada ya tukio la kijeshi la kuvikwa cheo kipya Sajini Bacca, amesema: “Sina budi kushukuru kikosi changu kwa kuweza kunisapoti kwa kila hatua. Nitaendelea kuipambania nchi yangu.”

KMKM iliyomwachia Bacca kuitumikia Yanga, ni kikosi cha ulinzi cha Zanzibar ambacho kina jukumu la kulinda mipaka ya bahari dhidi ya magendo, uvuvi haramu na vitendo vingine vya kihalifu.

Pia, KMKM husaidia katika operesheni za uokoaji baharini na usalama wa majini.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *