Benki ya Dunia yaipongeza Tanzania kwa mapinduzi sekta ya elimu

Benki ya Dunia imeipongeza Serikali ya Tanzania kwa mageuzi makubwa na mafanikio katika sekta ya elimu, hatua ambayo imewezesha watoto wa Kitanzania kupata elimu bila vikwazo vya aina yoyote.

Pongezi hizo zimetolewa Machi 16, 2025, jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Victoria Kakwa, alipotembelea Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa EASTRIP

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bi, Kakwa alisema kuwa Tanzania imejipambanua barani Afrika kwa kujikita katika kuboresha elimu.

Ameweka wazi kuwa jitihada hizi zimepelekea ongezeko kubwa la udahili wa wanafunzi katika ngazi zote za elimu na kupongeza uamuzi wa kurudisha watoto waliokuwa wamekatisha masomo kwa sababu mbalimbali kuendelea na masomo,

Ameeleza kufurahishwa kwake na utekelezaji wa Mradi wa EASTRIP katika DIT ambapo amesema amefurahushwa nanubunifu na umahiri wa vijana wa kitanzania katika eneonla TЕНАМА.

Kwa mujibu wa Bi. Kakwa, mradi wa EASTRIP umekuwa na mchango mkubwa katika kuleta mageuzi ya kielimu, hasa katika masomo ya ufundi na teknolojia, ambayo ni nguzo muhimu kwa kukuza ajira, kulinda mazingira na na uchumi wa nchi kwa ujumla. Aliongeza kuwa juhudi hizo zinaakisi dhamira ya Tanzania kufikia uchumi wa Viwanda na kujenga misingi imara ya maendeleo endelevu.

Mradi wa EASTRIP, unafadhiliwa na Benki ya Dunia, umewezesha uboreshahi Vyuo vya Ufundi na Teknolojia nchini. Tangu kuanzishwa kwake, mradi huu umeimarisha uwezo wa wakufunzi katika maeneo ya teknolojia na ubunifu, sambamba na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na fani za ufundi.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alisisitiza kuwa EASTRIP ni sehemu ya mpango mkubwa wa Serikali wa kuhakikisha elimu inakuwa jumuishi na yenye viwango vya kimataifa.Pia ameishukuru Benki ya Dunia kwa msaada wake endelevu na amewataka vijana wa Kitanzania kutumia kikamilifu fursa za mafunzo na ujuzi zinazotokana kupitia mradi huo.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *