Umoja wa walimu wasio na ajira (Neto) wa kati ya mwaka 2015 – 2023 umewasilisha mambo 6 katika kikao cha mawaziri wawili, moja ya mambo hayo ni ikiwemo kupunguza umri wa kustaafu kwa walimu kutoka miaka 60 hadi 50 ili kutoa nafasi za ajira kwa vijana Serikalini.
Mambo mengine yaliyowasilishwa ni pamoja na masuala ya mtaala mpya, usaili wa ajira za walimu, uzalishaji wa walimu, hali ya maisha ya walimu wasio na ajira mitaani na uhaba wa walimu.
Mkutano huo uliwakutanisha viongozi hao na mawaziri wawili ambao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.
Aidha Serikali imekubaliana kuunda timu ya wataalamu kutoka wizara tano kushughulikia changamoto za walimu hao, huku wakiombwa kuwa wavumilivu kwa kipindi cha siku 30 hadi 45 wakati swala lao linapofanyiwa kazi.