Arsenal imeonyesha dhamira ya kuimarisha safu yake ya kiungo kwa kuwaongeza Bruno Guimarães wa Newcastle United na Martin Zubimendi wa Real Sociedad.Hii ni moja ya hatua za kwanza za mkurugenzi mpya wa michezo, Andrea Berta.
Guimarães alijiunga na Newcastle Januari 2022 na amekuwa mhimili wa kikosi hicho, akiwasaidia kufuzu Ligi ya Mabingwa. Aliongeza mkataba wake hadi 2028, huku awali ikidaiwa ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 100.
Hata hivyo, taarifa mpya zinaonyesha kipengele hicho kimeondolewa, na hivyo uhamisho wake utategemea makubaliano na Newcastle.Arsenal inatarajia kumnasa kwa pauni milioni 60 ikiwa Newcastle haitafuzu kwa Ligi ya Mabingwa.
Zubimendi, anayesifika kwa uwezo wake wa kudhibiti mchezo, ana kipengele cha kuachiliwa cha €60 milioni katika mkataba wake na Real Sociedad.Arsenal inajaribu kushusha bei hiyo ili kuhakikisha usajili wake unakamilika.
Anahusishwa pia na Barcelona na Bayern Munich, lakini Arsenal ina matumaini ya kumnasa ili kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Mikel Arteta.
Chini ya uongozi wa Berta, Arsenal inataka kujenga kikosi chenye ushindani wa hali ya juu huku wakihitaji viungo wenye uwezo wa kucheza kwa kiwango cha juu dhidi ya wapinzani wakubwa.