Kocha mkuu wa klabu ya Atlético de Madrid Diego Simeone amesema kuwa kilichofanyika kwenye mchezo wa Jana dhidi ya Real Madrid C.F. ni upuuzi tu ulifanyika.
Diego Simione amenukuliwa akisema “Kwenye maisha yangu toka niwe kocha sijawahi kuona VAR inatumika kwenye mikwaju ya penalty.”
“Ni sheria mpya? Imetambulishwa lini? Haman la maana zaidi ya upuuzi tu.”
Atletico Madrid ilijikuta ikitolewa kwa mikwaju ya penati huku penat ya Julian Alvarez ikifutwa baada ya kusemekana amegusa mpira na miguu miwili hivyo kufanya mchezo huo kumalizika kwa Real Madrid kushinda 4-1 kwa mikwaju ya penati.