Jeshi la polisi la mshikilia Bondia Hassan mwakinyo

Jeshi la Polisi mkoani Tanga limeeleza sababu za kuendelea kumshikilia bondia maarufu wa Tanzania, Hassan Mwakinyo (29), anayekabiliwa na tuhuma za kumsambulia na kumjeruhi mkazi wa jiji hilo, Mussa Ally, kwa madai ya kumhisi kuwa mwizi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu, Machi 10, 2025, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi, alisema Mwakinyo anadaiwa kumshambulia Mussa Ally, ambaye ni mvuvi, wakati alipokuwa akipita karibu na makazi yake.

Kamanda Mchunguzi alifafanua kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea na mara utakapokamilika, Mwakinyo atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.”Mtuhumiwa amekamatwa kwa tuhuma za kumjeruhi mvuvi, ambalo ni kosa la jinai.

Sheria inapaswa kufuata mkondo wake bila kujali nafasi au umaarufu wa mtu katika jamii. Hakuna atakayekuwa juu ya sheria,” alisema Kamanda Mchunguzi.

Alisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litatoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari mara uchunguzi utakapokamilika na hatua zaidi za kisheria zitakapochukuliwa dhidi ya mtuhumiwa.Kwa sasa, Mwakinyo anashikiliwa katika kituo cha polisi huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini ukweli wa tukio hilo.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *