Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru jijini Arusha imepokea mashine ya kisasa ya mammografia itakayosaidia utambuzi wa saratani ya matiti ili kukokoa vifo vya wanawake wengi wanaofariki kwa ugonjwa huo.
Mtaalamu wa Radiologia katika hospitali ya Mount Meru Dkt. Edward Joseph amesema “Utambuzi wa mapema ni hatua muhimu kwa mafanikio ya matibabu na kuongeza uwezekano wa mgonjwa kupona,”.
Takwimu zinaonyesha kuwa wanawake 42,000 hugundulika kuwa na saratani ya matiti kila mwaka huku asilimia 38 pekee ya wagonjwa wanaopafa matibabu hupona. Mashine ya mammografia imetolewa na Serikali kukabidhiwa kitengo cha mionzi cha hospitali hiyo.