Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda amekemea vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na watu wanaodai kuwa na uwezo wa kusamehe madeni ya kodi.
Mwenda ametoa onyo hilo baada ya jeshi la polisi kukamata watuhumiwa wawili wanaodaiwa kufanya udanganyifu kuwa wao ni maofisa wa TRA na kuwa wanauwezo wakusamehe madeni ya kodi.
Mwendo amesema kuwa hakuna yeyote hata mtumishi wa TRA anayeweza kufuta madeni ya kodi, madeni hayo yanafutwa kwa kulipwa.
Mwenda amewaonya wananchi na walipa kodi kutoamini watu wanaodai kuwa na uwezo huo akisisitiza kuwa ni uongo na utapeli.