Nyota wa ngumi Ryan Garcia alikiri siku ya Jumanne wiki hii kwamba haikuwa jambo jema kunywa pombe na kuvuta bangi kabla ya pambano lake la Aprili 2024 dhidi ya Devin Haney.
Garcia aliposti video kwenye mitandao ya kijamii siku chache kabla ya pambano hilo la uzito wa junior welterweight – ambalo alishinda kwa uamuzi wa majaji wengi – akionyesha akinywa kwenye klabu. Pia, aliigiza kunywa bia wakati wa kupima uzito.
Licha ya tabia yake isiyo pendeza katika mtazamo wa kijamii, Garcia alimwangusha Haney mwenye rekodi ya (31-0, 15 KOs) mara tatu katika ushindi uliotikisa wengi. Hata hivyo, baadaye Garcia alipatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni, na matokeo yake yalibatilishwa kuwa “no-contest”. Pia, alipigwa marufuku kwa mwaka mmoja na Tume ya Michezo ya Jimbo la New York.
Garcia mwenye rekodi ya (24-1, 20 KOs) atamaliza yake hiyo hivi karibuni na atapambana na Rolly Romero mnamo Mei 2, katika pambano litakalofanyika nje kwenye eneo la Times Square. Hili litakuwa pambano kuu kwenye onyesho la Ring Magazine, likijumuisha pia kurejea kwa Haney dhidi ya Jose Ramirez na Teofimo Lopez akitetea taji lake la uzito wa 140 dhidi ya Arnold Barboza Jr.”Nataka kuwa bora,” alisema Garcia. “Nimekuwa nikitaka kupigana na mabondia bora kwenye mchezo huu.
Kuhusu matatizo yangu nje ya ulingo, nimekuwa nayo daima. Sijui nani mwingine anayekabiliana na mambo kama haya, lakini ni kitu ambacho nimekuwa nikihangaika nacho.”