Watu 53 wafariki kwa ugonjwa usiojulikana Congo.

Madaktari wa Shirika la Afya duniani (WHO) wamethibitisha kuwa zaidi ya watu 50 wamefariki kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ugonjwa usiojulikana.

Mkurugenzi wa hospitali ya Bikoro, Serge Ngalebeto amesema kuwa muda kati ya kuanza kwa dalili na kifo ni masaa 48 kwa wagonjwa wengi huku hali hiyo ikitia wasiwasi.

Mlipuko wa ugonjwa huo usiojulikana ulitokea Januari 21 na hadi sasa kuna wagonjwa 419 ikiwemo vifo vya watu 53.

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya duniani lililopo Afrika mlipuko wa kwanza wa ugonjwa huo ulitokea katika mji wa Boloko baada ya watoto watatu kula popo na kufariki baada ya masaa 48.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *