Tanzania kuingiza bilioni 2.5 uwindaji wa kitalii

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kuingiza jumla ya Dola za Kimarekani 968,000 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 2.5 kama ada ya vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa mwaka bila mapato mengine.

Hayo yamesemwa leo Februari 21,2025 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti vya umiliki wa Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii kwa wawekezaji watano (5), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Ninayo furaha kukabidhi vyeti hivi kwa wawekezaji ambao ni K&F Wild Expedition Ltd (kwa kitalu cha Kilwa Open Area Nakiu), Michel Mantheakis Safaris Ltd kwa (Muhesi GR), Out of Africa Ltd (Lwafi Nkamba), Royal Conservation Ltd (Pololeti GR), na Neon Investment Ltd (Selous MT2) chini ya Uwekezaji Mahiri kwenye Maeneo ya Wanyamapori (Special Wildlife Investment Concession Areas-SWICA)” amesisitiza Mhe. Chana.

Amefafanua kuwa utoaji wa vyeti hivyo kwa wawekezaji hao wapya unaendana na utekelezaji wa Ilani ya CCM, kutokana na ukweli kwamba hiyo inahalalisha umuhimu wa tasnia ya uwindaji kwa uchumi wa nchi na kusisitiza kuwa Uwindaji wa Kitalii unachangia manufaa ya moja kwa moja kupitia ajira na maendeleo kwa jamii.

Mhe. Chana ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wengine kutoka China na kwingineko duniani kuwekeza katika Sekta ya Utalii nchini Tanzania huku akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Mpango wa kuitangaza Tanzania katika kiwango cha kimataifa kupitia filamu za “Amazing Tanzania” na “Tanzania, The Royal Tour”

Ninapenda kuwahakikishia wadau wote wa uwindaji wa Kitalii kwamba dhamira ya Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuendelea kuweka na kudumisha mazingira wezeshi ya biashara zao bila kuathiri uhifadhi na ustawi wa watu wetu” amesema Mhe. Chana.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *