Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) Tanzania Bara, Innocent Siriwa ametangaza nia ya kuwania Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.
Siriwa ametaja vipaumbele vitano ambayo atavipambania endapo Chama chake kitampotisha kuwania nafasi hiyo. Vipaumbele hivyo ni pamoja na elimu bure, afya bure, katiba mpya, ajira kwa vijana na Tanzania ya kidijitali.