Tanesco yatolea ufafanuzi taarifa ya kukosekana kwa umeme.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewatoa hofu wananchi kuwa maboresho yatakayofanyika kwanzia Februari 22-28 hayatafanyika kwa siku 6 mfululizo na hayatawaathiri wananchi kwa muda wote.

Tanesco wametoa ufafanuzi kwa kusema “Tutakuwa na maboresho ya miundombinu yatakayofanyika katika kituo cha kupokea, kupoza na kusafirisha umeme cha Ubungo ambayo yanaweza kuathiri upatikanaji wa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti kwenye baadhi ya maeneo ya Zanzibar, Dar na Pwani,”.

“Tunapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa maboresho hayo hayatakuwa kwa siku 6 mfululizo na hayatawaathiri wananchi kwa muda wote, Shirika linafanya kila jitihada kuhakikisha athari zitakazotokana na maboresho hayo kuwa za kiwango cha chini kadri iwezekanavyo, tutendelea kuwataarifu maendeleo ya kazi hiyo mpaka itakapokamilika,”.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *