Shirikisho la soka Afrika (CAF) limepanga kufanya marekebisho makubwa ya mashindano yake hasa ligi ya mabingwa Afrika na kombe la Shirikisho la CAF.
CAF imekuwa ikichunguza njia za kuweka upya kandanda ya Afrika na kulingana na ripoti ya CAF inazingatia mfululizo wa mabadiliko ya kisasa na kuboresha muundo wa uuzaji na ushindani wa mashindano ya vilabu vyake.
Pendekezo la msingi linahusisha kufutiliwa mbali kwa kombe la Shirikisho la CAF na kurekebisha muundo wa ligi ya mabingwa kwa kupanua ligi ya mabingwa huku ikidumisha African Football League kama shindano kuu.