Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde amesema ujenzi wa viwanda vinne vya uchenjuaji madini ya Shaba ikiwemo kiwanda cha Shengde Precious Metal Resources Co. Limited kinachoendelea kujengwa katika eneo la Mahungu kata ya Nala Jijini Dodoma vinatarajiwa kuwa mkombozi wa wachimbaji wadogo wa madini ya Shaba nchini Tanzania.
Waziri Mavunde ameyazungumza hayo baada ya kutembelea na kukagua maendelo ya ujenzi wa kiwanda hicho na kutoa pongezi kwa kampuni ya Shengde Precious Metal Resources Co. Limited kwa uamuzi wa kujenga kiwanda hicho Jijini Dodoma.
Aidha Waziri Mavunde amesema Serikali imedhamiria kwa dhati kuyaongezea thamani madini hapa nchini ili kukuz ajira kwa watanzania na kuongeza pato la taifa ambapo amewaahidi kupatiwa ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini.
Mbali na Dodoma Waziri amesema ujenzi wa viwanda kuongeza thamani madini ya Shaba na Nikeli unaendlea maeneo mengi nchini ikiwemo Lindi na Mbeya na kutoa rai kwa mikoa kutenga maeneo maalum ya ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani madini.