Tanzania na Italy washiriki kongamano la uwekezaji

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeshiriki katika kongamano kubwa la uwekezaji kati ya Tanzania na Italy lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limehudhuriwa na zaidi ya washiriki 500, wakiwemo wawekezaji, maafisa wa serikali, na wadau mbalimbali wa biashara.

Lengo kuu la kongamano hilo lilikuwa ni kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italy, huku mada kuu zikihusisha mazingira rafiki ya uwekezaji katika sekta za afya, kilimo, na uchumi wa bluu. Majadiliano yalihusu fursa zilizopo, changamoto zinazokabili wawekezaji, na mikakati ya kuendelea kuboresha mazingira ya biashara kati ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Kombo, alieleza kuwa uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Italy umekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo nchini. Alisisitiza kuwa sekta ya uchumi inaendelea kukua kwa kasi kutokana na biashara na uwekezaji wa kimataifa, na akawakaribisha wawekezaji wa Italy kuendelea kuwekeza Tanzania.

Kwa upande wake, Balozi wa Italy nchini Tanzania, Giuseppe Coppola, alisema kuwa Italia itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali ili kuimarisha mahusiano ya kiuchumi. Alibainisha kuwa fursa zilizopo katika kilimo, afya, na uchumi wa bluu zinapaswa kutumiwa ipasavyo kwa manufaa ya pande zote mbili.

Kongamano hili ni sehemu ya juhudi endelevu za serikali ya Tanzania katika kuvutia wawekezaji wa kimataifa na kukuza uchumi wa nchi kupitia miradi yenye tija. Washiriki walipata nafasi ya kubadilishana mawazo, kushiriki majadiliano ya kina, na kuangazia mikakati inayoweza kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Italy.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *