Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba amebainisha kuwa bajeti ya serikali imekumbana na changamoto nyingi katika mwaka jana na mwaka huu akitoa maelezo hayo leo 11 February 2025 Bungeni Dodoma.
Uharibifu wa barabara uliosababishwa na hali ya hewa uliathiri miundombinu chini ya Wakala wa Barabara Vijijini (Tarura) na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) umechangia hali hii ngumu lakini pia changamoto za umeme zililazimu serikali kuchukua hatua za dharura kama vile kukodi mitambo na kuharakisha ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere.
Dk. Nchemba alisema “Mwaka jana, tulipata changamoto kubwa kutokana na uharibifu wa barabara na tatizo la umeme ambalo lilituathiri kwa kiasi kikubwa”
Dk. Nchemba alifafanua kuwa serikali ililipa zaidi ya Sh400 bilioni kwa mwezi ili kuhakikisha mradi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere unakamilika kwa wakati. Sasa baada ya kukamilika kwa mradi huo, Serikali imeanza kurejesha kasi ya utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo nchini