Msanii maarufu wa muziki wa Bongo Flava, Juma Mussa Mkambala, anayejulikana kama Juma Jux, amefunga ndoa na Priscilla Ojo, binti wa mwigizaji mashuhuri kutoka nchini Nigeria. Sherehe hiyo ya Kiislamu ilifanyika wiki hii jijini Dar es Salaam, ikihudhuriwa na mastaa wa muziki kutoka Tanzania akiwemo Diamond Platnumz, G nako, Ommy Dimpoz na wengine wengi kutoka Nigeria.
Lakini kabla ya Juma Jux kumpata Priscilla alikua mpenzi wa Vanessa Mdee mwanadada, ambaye alishawahi kufanya vizuri miaka ya 2012-2018 kabla ya kuachana kwa wawili hao.
Katika Hafla hiyo msanii Juma Jux pamoja na familia yake wameonyesha upendo wa hali ya juu kwasaabu wameupokea ugeni kutoka nchini Nigeria kwa upendo
Juma Jux alieleza kuwa aliamua kufunga ndoa kwa faragha, akihusisha familia na marafiki wa karibu pekee, ili kudumisha unyenyekevu na usiri katika tukio hilo muhimu maishani mwake.