Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Nicodemus Banduka amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80 katika hospitali ya Mloganzila Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.
Banduka anakumbukwa kama mmoja wa waasisi wa katiba ya CCM mwak 1977 inayotumika mpaka sasa vilevile amehuduma kama Mkuu wa Mkoa wa Mikoa mbalimbali ikiwemo Lindi, Pwani, Iringa, Ruvuma na Shinyanga.
Mwili wa marehemu Banduka utapokelewa kwa heshima tarehe 11/02/2025 katika kanisa la KKT Nyumbu, Kibaha na maziko yatafanyika kijijini kwakw Mruma Ugweno huko Kilimanjaro.