Rais wa kwanza wa Namibia, Sam Nujoma amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.
Sam Nujoma aliongoza mapambano ya kupigania uhuru wa Namibia kutoka utawala wa Afrika Kusini mwaka 1990 ilipopata uhuru.
Moja ya matukio yakukumbukwa kuhusu yeye ni mwaka 1960 alipokimbilia nchini Tanzania kutokana na vuguvugu lililotokea nchini Namibia ambapo Hayati Mwl. Nyerere alimpatia hifadhi.
Baada ya Namibia kupata uhuru alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo na kufanikiwa kudumu mpaka mwaka 2005 ambapo aliamua kustaafu.