TCRA yapata washindi shindano la Cyber Champions.

Shindano la Cyber Champions lililoandaliwa na kuratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) limepata washinidi wanne kati ya mia sita walioshiriki. Shindano hilo lilihusisha vyuo mbalimbali zaidi ya 40 kutoka taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini.

Washindi ni pamoja na Amani Nasemwa kutoka Chuo Kikuu cha UDOM aliyeshika nafasi ya kwanza, John Mange kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) aliyeshika nafasi ya pili, John Mpagama kutoka Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU) aliyeshika nafasi ya tatu na Rebecca Kubanda kutoka UDOM aliyeshinda kwa upande wa washiriki wa kike.

Mkurugenzi wa TCRA Dkt. Jabir Bakari amewakabidhi washindi hao zawadi ambazo ni kompyuta, pamoja na kufadhiliwa gharama za mafunzo vilevile zawadi zilizotolewa na Mamlaka ya Serikali mtandao (e-GA) ya kufanya internship katika kituo cha utafiti na ubunifu e-GA.

Shindano hilo lililenga kuibua vipaji, kuimarisha uelewa wa usalama mtandaoni wa kuwaandaa vijana kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *