Katika ligi ya kikapu nchini Marekani ya NBA, nyota wa Los Angeles Lakers, Lebron James ameiongoza timu hiyo kupata ushindi dhidi ya Golden State Warriors katika ligi ya NBA.
Kubwa kuliko kwenye mchezo huo ni nyota huyo kufunga pointi 42 ‘ribaundi’ 17 na Asisti 8 katika mchezo uliomfanya aungane na nguli wa mchezo huo Michael Jordan ya kuwa wachezaji pekee waliowahi kufunga pointi zaidi ya 40 katika mchezo mmoja wakiwa na umri wa miaka 40 katika ligi ya NBA.
Michael Jordan aliweka rekodi hiyo mwaka 2003 alipokuwa Washington Wizards akifunga pointi 43 dhidi ya New Jersey Nets.