Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ajulikanaye kama Duduzile Zuma Sambudia amefikishwa mahakamani baada ya kushtakiwa kuchochea vurugu wakati wa ghasia za mwaka 2021 nchini Afrika Kusini ambapo zaidi ya watu 300 walipoteza maisha.
Licha ya wakili wa binti Zuma amekana mashtaka hayo waendesha mashtaka wanadai kuwa Duduzile alichochea watu wengine kufanya vurugu katika machapisho kupitia mitandao ya kijamii mwaka 2021 wakati machafuko yalipozuka baada ya baba yake kukamatwa kwa kutotii amri ya mahakama ya kutoa ushahidi kuhusiana na kashfa ya ufisadi iliyokuwa inamkabili.