Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Bw. Mkama Bwire amesema ujenzi wa mradi wa bwawa la Kidunda Mkoani Morogoro unatarajiwa kumaliza tatizo la maji Mkoa wa Dar-Es-Salaam.
Mkama Bwire ameyasema hayo katika ziara ya jukwaa la wahariri (TEF) na waandishi wa habari kujionea maendeleo ya mradi huo wa bwawa ulipofikia.
Mradi huo unaosemekana kufikia asilimia 27 ya ujenzi wake umeigharimu Serikali kiasi cha shilingi bilioni 336 kutoka mapato ya ndani. Mradi huo unatarajiwa kukamalika ndani ya kipindi cha miaka mitatu kwanzia June 18, 2023 mpaka Desembe 2026 na utasimamiwa na Dawasa kupitia Wizara ya Maji.