Presha inazidi kupanda kwa kocha Mikel Arteta baada ya timu hiyo kutolewa kwenye michuano ya Carabao hapo jana. Mchezo huo uliokuwa na nusu fainali ulishuhudia Arsenal ikifungwa 2-0 dhidi ya Newcastle ambao waliwafunga uwanja wao wa nyumbani wiki 2 zilizopita na kufanya matokeo kuwa 4-0 kwa ujumla.

Mashabiki wa timu hiyo wameanza kupoteza imani na kocha wao ikiwa ndani ya miaka mitano aliyodumu alifanikiwa kushinda kombe moja tu la FA na ngao za hisani mbili. Mashabiki hao pia wameonyesha kuilaumu bodi yao kutofanya usajili wowote dirisha la Januari.

Matumaini ya Arsenal kutetea msimu wao yamebaki kwenye ligi kuu nchini Uingereza pamoja na Ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Katika habari nyingine ya kusikitisha kwa Arsenal ni winga Gabriel Martineli anatarajiwa kukosekana michezo kadhaa baada ya kupata majeruhi ya misuli katika mchezo huo dhidi ya Newcastle United.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *