FCS na SIDO kushirikiana kuwawezesha kiuchumi makundi maalum.

Shirika la The Foundation For Civil Society FCS limetia saini makubaliano ya kushirikiana kati yake na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) kutekeleza mradi wa miaka mitatu wa kuwawezesha kiuchumi makundi maalum ya Vijana, wanawake na watu wenye Ulemavu.

Akizungumza katika hafla fupi yakutia saini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge amesema kuwa Mkataba huo unakwenda kuhakikisha fursa mbalimbali zinazopatikana katika Taifa, haziachi nyuma makundi maalum.

“Tunaingia makubaliano na SIDO ili kuwezesha makundi haya kutumia vizuri zaidi fursa mbalimbali zinazopatikana katika Shirika hili, ambalo ni muhimu sana katika maendeleo ya Viwanda, Ujasiriamali na uzalishaji mali kwa ujumla” amesema Rutenge.

Kwa muda mrefu FCS toka kuanzishwa kwake imekuwa wakifanyakazi zilizolenga kutetea haki, katika mpango mkakati wake, wameweka haki za uchumi kama sehemu muhimu ya kazi zake ikiwemo kuhakikisha fursa zinazopatikana katika ngazi mbalimbali zinawafikia walengwa, ili kuongeza thamani katika shughuli zao.Aidha kwa upande wake Meneja wa SIDO Mkoa wa Dar es Salaam, Hopeness Elia, amesema muungano uliopo kati yao na FCS unaenda kuongeza nguvu na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuiwezesha jamii kufikia malengo ya kiuchumi.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *