Trump kuondoa tishio la kodi kwa Mexico na Canada

Rais wa Marekani Donald Trump amesitisha tishio lake la ushuru mkubwa kwa Mexico na canada siku ya Jumatatu, akikubali kusitisha kwa siku 30 baada ya kurudiwa kwa makubaliano kuhusu utekelezaji wa maswala ya mipaka na uhalifu baina yake na nchi hizo mbili jirani.

Hata hivyo, ushuru wa Marekani kwa China bado unatarajiwa kuanza kutumika ndani ya saa chache.Waziri Mkuu wa canada Justin Trudeau na Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum walisema wamekubali kuimarisha juhudi za utekelezaji wa sheria mipakani ili kukabiliana na shinikizo la Trump la kupambana na uhamiaji haramu na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Hatua hiyo itasitisha ushuru wa 25% uliopaswa kuanza kutumika Jumanne kwa muda wa siku 30.Canada ilikubali kutumia teknolojia mpya na kuongeza wafanyakazi katika mpaka wake na Marekani, pamoja na kuzindua juhudi za pamoja za kupambana na uhalifu uliopangwa, usafirishaji haramu na utakatishaji wa fedha.

Mexico ilikubali kuimarisha mpaka wake wa kaskazini kwa kupeleka wanachama 10,000 wa Walinzi wa Kitaifa ili kudhibiti mtiririko wa uhamiaji haramu na dawa za kulevya.Marekani pia iliahidi kuzuia usafirishaji wa silaha zenye nguvu kubwa kuelekea Mexico, Sheinbaum alisema.”Kama Rais, ni jukumu langu kuhakikisha usalama wa Wamarekani WOTE, na ninafanya hivyo. Ninafurahia matokeo haya ya awali,” Trump alisema kwenye mitandao ya kijamii.

Makubaliano haya yanazuia kwa sasa kuanza kwa vita vya kibiashara ambavyo wataalam wa uchumi walitabiri vingeharibu uchumi wa pande zote na kusababisha kupanda kwa bei kwa watumiaji.Baada ya kuzungumza kwa simu na viongozi wote wawili, Trump alisema atajaribu kujadili makubaliano ya kiuchumi katika mwezi ujao na washirika wawili wakubwa wa biashara wa Marekani, ambao uchumi wao umeunganishwa kwa karibu na Marekani tangu mkataba mkubwa wa biashara huria ulipofikiwa katika miaka ya 1990.

Ikiwa mpaka sasa bado hakuna makubaliano yaliyofikiwa kwa China, ambayo inakabiliwa na ushuru wa 10% kwa bidhaa zote unaotarajiwa kuanza saa 6:01 asubuhi Jumanne saa za Afrika Mashariki, Msemaji wa Ikulu ya Marekani alisema Trump hatokuwa na mazungumzo na Rais wa China Xi Jinping hadi baadaye katika wiki hiyo.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *