Uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unapanga kukutana kwenye mkutano wa kutafuta suluhisho la mgogoro mwa Mashariki mwa Congo. Kikao kinachotarajia kufanyika Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye ni Rais wa Kenya Mhe. William Ruto ambapo amesema Rais wa Tanzania, Uganda, Afrika Kusini, Somalia, Congo na Rwanda wamethibitisha kushirki kikao hicho.
Rais Ruto amesema kwa kushirikiana pamoja watahakikisha amani inarejea na kutawala baina ya nchi zote za jumuiya hizo.