Benki ya Dunia imesema ipo tayari kutoa mitaji, dhamana na usaidizi wowote ili kuhakikisha sekta binafsi inakuwa kipaumbele katika kuwasaidia vijana wa Afrikia kufikia ndoto zao na maono yao kwa kuwekeza kwenye sekta ya nishati.
Hayo yamezungumzwa na Rais wa Benki ya Dunia Bw. Ajay Banga katika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu Nishati jijini Dar Es Salaam.
“Sekta binafsi ni wadau muhimu wanapaswa kuwekeza katika mazingira ambayo watajiamini katika uwekezaji wao, wanahitaji kuwekeza katika mazingira yenye uwajibikaji”
“Benki Kuu ipo tayati kutoa, mitaji dhamana na usaidizi wowote ili kuhakikisha sekta binafsi inakuwa kipaumbele kwasababu peke yenu hamuwezi kufanikiwa, tunatarajia kupata fedha kwaajili ya kuwezesha kwa miaka mitano au sita ijayo, Benki ya Dunia itawekeza fedha nyingi, kama tutaweka dolla billioni 100 katika miradi hii, fedha hizi zikiwekezwa katika katika jitihada hizi kuwasaidia Wananchi wa Afrika kufikia ndoto zao na maono yao hichi ndicho kipaumbele kikubwa,”. Alisema.