Taifa Stars ndani ya kundi C fainali za Afcon 2025.

TANZANIA imepangwa Kundi C katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zitakazofanyika kuanzia Desemba 21 mwaka huu hadi Januari 18 mwakani, 2026 pamoja na jirani zao, Uganda, Tunisia na Nigeria.

Katika Droo ya upangaji makundi ya AFCON 2025 iliyofanyika usiku wa Jumatatu ukumbi wa Mohammed V National Theatre Jijini Rabat nchini Morocco, wenyeji wa Fainali hizo wapo Kundi A pamoja na Mali, Zambia na Comoro, wakati mabingwa watetezi, Ivory Coast wapo Kindi F pamoja na Cameroon, Gabon na Msumbiji.

Kundi B linazikutanisha Misri, Afrika Kusini, Angola na Zimbabwe, wakati D kuja Senegal, DRC, Benin na Botswana na Kundi E wapo Algeria, Burkina Faso, Equatorial Guinea na Sudan.

Timu ya Taifa ya Tanzania, maarufu kama Taifa Stars, imefuzu kwa mara ya nne kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika nchini Morocco.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufuzu kwa AFCON mara mbili mfululizo, baada ya kushiriki katika michuano ya 2023. Kwa sasa, Tanzania inajiandaa kwa michuano hiyo mikubwa barani Afrika, ikilenga kufanya vizuri zaidi na kuvuka hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *