Serikali yafanya ujenzi wa vituo vya Gesi ya Magari

Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imepongezwa kwa ujenzi wa mradi wa Kituo mama cha gesi iliyoshindiliwa yaani Compressed Natural Gas (CNG) na Vituo vidogo viwili vya kupokea na kuhifadhi CNG kwa wateja wa awali.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. David Mathayo David wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa kituo hicho cha kujazia gesi kinachojengwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na kujionea maendeleo ya kituo cha kupokea gesi asilia cha Kinyerezi.

“Tunaipongeza Serikali kwa kupokea ushauri wa Bunge kwa kujenga kituo hiki kikubwa cha kujazia gesi kwenye magari ambacho kitasaidia vituo vingine vidogo kuchukua gesi katika kituo hiki ili kwenda kujaza magari katika maeneo mengine,” amesema Mhe. David

Aidha, Kamati ya Bunge imeishauri Serikali kufikiria namna bora ya kusambaza miundombinu ya kusafirisha gesi ili iweze kufika maeneo mengi nchini ili kuendelea kuwapatia fursa wananchi kuendesha mitambo kwa kutumia gesi asilia badala ya mafuta kama ilivyozoeleka.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *