TIC yashiriki jukwaa la Uwekezaji na Biashara Misri

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na ZIPA na Ubalozi wa Tanzania nchini Misri wameweza kuandaa na kufanikisha Jukwaa la Biashara na Uwekezaji baina nchi hizi mbili.

Jukwaa hili limefanyika tarehe 23 Januari 2025 katika Hoteli ya Conrad jijini Cairo na kuhudhuriwa na zaidi ya wafanyabiashara na wawekezaji mia moja (100) kutoka Misri na ujumbe wa Tanzania kutoka sekta ya binafsi na ya umma takribani thelathini (30) ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dk. Stephen J. Nindi.

Lengo la Jukwaa hili lilikuwa kuelezea fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania ili kuvutia makampuni mengi ya uwekezaji kutoka Misri kuja kuwekeza nchini hususan katika sekta za kilimo, nishati, ujenzi wa majumba, viwanda, benki na fedha, utalii na miundombinu.

Katika Jukwaa hili wasilisho la TIC lililohusu mazingira ya biashara na fursa za uwekezaji lilifanywa na Bw. Daudi Riganda, Meneja Uhamasishaji Uwekezaji wa Nje. Aidha, TIC iliweza kushiriki katika mikutano ya ana kwa ana ya kibiashara (B2B meetings) na kampuni kadhaa za Misri

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *