Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imemkabidhi tuzo ya kumshukuru kuunga mkono uhamasishaji wa ulipaji kodi kwa hiari na kurahisisha ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2023/2024, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tuzo hizi zimefanyika katika maadhimisho ya siku ya mlipa kodi katika ukumbi wa Superdome Masaki, jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Vilevile Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda ametaja vigezo vitano vilivyotumika kupata washindi wa tuzo hizo kuwa ni mlipaji kodi mwenye rekodi nzuri katika ulipaji wa kodi, mlipa kodi anayelipa kwa hiari kwa wakati, mlipa kodi anayetumia EFD Machine na VFD kikamilifu, mlipa kodi anayelipa kodi kubwa zaidi na mlipa kodi anayetoa ushirikiano na TRA.
Aidha tuzo hizo zimeshuhudia beki ya NMB ikipokea tuzo ya ulipaji kodi bora kwa mwaka 2023/2024. NMB wanatajwa kuwa walipaji kodi wa hiari.