Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Tundu Lissu amemteua John Mnyika kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho akiwa katika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama.
Mhe. Tundu Lissu pia ameteua Manaibu Katibu Wakuu wa Chama kama ifuatavyo Wakili Ally Ibrahim Juma kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar pamoja na Aman Golugwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara.
Aidha amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ambao ni Godbless Lema, Dkt. Rugemeleza Nshala ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chama, Rose Mayemba, Salma Musa Kasanzu na Hafidh Ally Salehe.