Rais Donald Trump alitangaza mpango mkubwa wa kuendeleza miundombinu ya akili bandia ya Marekani, kupitia mradi unaoitwa Stargate.Ukiongozwa na OpenAI, SoftBank, na Oracle.
Mradi huu unatarajiwa kuvutia hadi uwekezaji wa kibinafsi wa dola bilioni 500 ndani ya miaka minne, ikijumuisha ujenzi wa vituo vya data huko Texas.
Trump alisema juhudi hii inaweza kuleta zaidi ya ajira mpya 100,000 kwa muda mfupi, huku ikiweka Marekani katika nafasi ya kushindana na mataifa kama China.
Viongozi wa miradi hii pia walionyesha matumaini kwamba mpango huu utaharakisha ugunduzi wa matibabu, ikiwezekana kutibu magonjwa kwa kasi zaidi ya hapo awali.