Mgombe Uenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amempomgeza Tundu Lissu na wenzake kwa ushindi katika Uchaguzi uliofanyika wa kupata viongozi wapya wa Chama hicho.
Licha ya kwamba matokeo bado hayajatangazwa Freeman Mbowe kupitia ukurasa wake wa X amempongeza Tundu Lissu akiashiria ndiye mshindi wa nafasi ya Uenyekiti wa Chama hicho katika uchaguzi huo huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikiwa ya John Heche.