Dkt.Biteko ahimiza mitaala vyuoni kuendana na mabadiliko ya teknolojia

Vyuo na taasisi zinazotoa elimu ngazi ya Kati ikiwemo Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), zimetakiwa kuboresha mitaala yake ya masomo ili iendane na mahitaji ya sasa ya soko la ajira kimataifa sambamba na mahitaji ya kijamii na kiuchumi.

Hayo yamebainishwa leo Januari 21, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko katika Maadhimisho ya miaka 60 ya chuo hicho kilichoanzishwa Januari 21, 1965.”Serikali inasisitiza matumizi ya teknolojia za kisasa na mbinu za kujifunza zinazojibu changamoto za kimataifa, ” Amesema Dkt. Biteko.

Amesema kuwa Serikali inazitaka taasisi za elimu ya kati kikiwemo Chuo cha CBE kuweka mkazo kwenye mafunzo ya ujasiriamali, ili wahitimu wake waweze kuchangia kikamilifu katika uchumi wa taifa kupitia biashara bunifu na ajira binafsi.

Aidha, taasisi za elimu, zikiwemo vyuo kama CBE, amezitaka kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi ili kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanakidhi mahitaji ya soko la ajira na pia kusaidia kukuza sekta hiyo kwa utafiti na mafunzo.

Ameongeza kuwa, Serikali inahimiza vyuo vya elimu ya biashara kufanya tafiti za kina zinazosaidia kutatua changamoto za kiuchumi, kuimarisha sera za biashara, na kubuni suluhisho endelevu.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *