Tanapa yatoa mafunzo ya kudhibiti mioto kichaa kwa JWTz

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) jana Januari 20, 2025 limeendesha mafunzo maalum kwa Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) jinsi ya kudhibiti mioto kichaa inayotokea ndani ya Hifadhi za Taifa inayosababishwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu kama vile ujangili na utayarishaji wa mashamba unaotekeleza na wananchi wanaopakana na hifadhi hizo.

Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa Mikumi kwa Wanajeshi wa Kikosi cha Usafiri wa Anga 603 KJ kutoka Dar es Salaam yalilenga kuleta ufanisi wakati wa kukabiliana na majanga ya moto yanapotokea ndani na nje ya Hifadhi za Taifa Tanzania.

Akitoa mafunzo hayo kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi -TANAPA, Afisa Uhifadhi Daraja la Kwanza Samwel Mgohach alisema, “Mioto Kichaa ni moja ya changamoto zinazotukabili katika hifadhi zetu kwani huathiri viumbe hai wengi sana hususani wale wanaotambaa na wanyama wenye mimba na wale wenye ndama wadogo ambao hawawezi kukimbia kipindi moto unapochachamaa.”

Aidha, mioto hii pia imeendelea kuathiri ikolojia ya hifadhi na maeneo yaliyohifadhiwa na kusababisha baadhi ya viumbe kutoweka katika ardhi ya Tanzania, hata hivyo mioto hii huongeza kasi ya mabadiliko ya tabianchi ambayo madhara yake ni pamoja na ukame, kuongezeka kwa joto duniani na matetemeko ya ardhi, aliongeza Afisa Uhifadhi Mgoach.

Mioto ambayo imeendelea kulikumba Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania na maeneo mengine nchini ni pamoja na “surface fire” ambao husambaa juu ya tabaka la ardhi kwa kuunguza majani na nyasi lakini hauna madhara makubwa kwa mizizi na tabaka la udongo, aina nyingine ni “Crown fire na Ground fire” ambao hutambaa chini kwa ukiathiri mizizi na mashina ya miti.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *