IMF yatabiri kukua kwa uchumi mwaka 2025.

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linatarajia uchumi wa dunia kukua kwa kasi kidogo zaidi huku mfumuko wa bei ukitarajiwa kuendelea kushuka mwaka huu. Hata hivyo, limeonya kuwa hali ya uchumi kuathiriwa na ahadi za Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, za kupunguza kodi za Marekani, kuweka ushuru kwenye bidhaa za nje, kulegeza kanuni za biashara, na kuwafukuza mamilioni ya wahamiaji wanaofanya kazi kinyume cha sheria nchini Marekani.

Shirika hilo lenye makao yake mjini Washington linatarajia uchumi wa dunia kukua kwa 3.3% mwaka huu na mwaka ujao, kutoka 3.2% mwaka 2024. Ukuaji huu ni wa wastani lakini haujafika kiwango cha juu sana. Kuanzia mwaka 2000 hadi 2019, uchumi wa dunia ulikua kwa wastani wa 3.7% kwa mwaka. Ukuaji huu dhaifu unaakithi athari za majanga makubwa ya kimataifa, ikiwemo janga la COVID-19 na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

IMF ni shirika lenye wanachama 191 linalofanya kazi ya kukuza ukuaji wa uchumi, kuimarisha usalama wa kifedha, na kupunguza umasikini duniani.

Mfumuko wa bei wa kimataifa, ambao uliongezeka baada ya janga la COVID-19 ulivuruga minyororo ya ugavi na kusababisha uhaba wa bidhaa na kupanda kwa bei, unatarajiwa kushuka kutoka 5.7% mwaka 2024 hadi 4.2% mwaka huu na 3.5% mwaka 2026.

Lakini, katika chapisho la blogi lililoambatana na ripoti ya karibuni ya IMF kuhusu Mtazamo wa Uchumi wa Dunia, mchumi mkuu wa shirika hilo, Pierre-Olivier Gourinchas, aliandika kuwa sera ambazo Trump amepanga kuanzisha “zinaweza kuongeza mfumuko wa bei kwa muda mfupi.”

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *