Makampuni barani Afrika hayana imani na usalama wa mitandao

Angalau kampuni nne kati ya kumi barani Afrika hazina imani na maandalizi ya serikali zao kukabiliana na tukio kubwa la usalama wa mtandao, ikiwa ni asilimia ya juu zaidi ikilinganishwa na maeneo mengine duniani. Matokeo haya yanaweza kuonyesha uwekezaji duni wa kitaifa katika usalama wa mtandao kote barani.

Hii inamaanisha kuwa idadi kubwa ya mashirika barani humo yanahofia kuwa iwapo kutatokea shambulio kubwa la kimtandao, yanaweza kupata hasara kubwa za kiuchumi na madhara mengine kwa sababu serikali zao hazina mikakati ya kutosha kupunguza athari za matukio hayo.

Ripoti ya hivi karibuni ya Global Cybersecurity Outlook iliyochapishwa na World Economic Forum wiki hii inaonyesha kuwa ingawa kampuni nyingi hazina imani na maandalizi ya kitaifa ya usalama wa mtandao, mashirika barani Afrika yana wasiwasi zaidi.

Kulingana na utafiti uliofanywa na taasisi hiyo ya kimataifa, asilimia 36 ya kampuni barani Afrika hazina imani na maandalizi ya nchi zao kushughulikia matukio ya usalama wa mtandao, ikilinganishwa na asilimia 15 tu huko Ulaya na Amerika Kaskazini, na sifuri katika ukanda wa Oceania.

Ni asilimia tisa tu ya mashirika barani Afrika ambayo yana “imani kubwa” katika maandalizi ya serikali zao kuhusu usalama wa mtandao, huku asilimia hiyo ikipanda hadi 13, 17, na 25 katika maeneo ya Ulaya, Amerika Kaskazini, na Oceania mtawalia.

Wataalamu wa sekta hiyo wanasema hawajashangazwa na matokeo haya, kwani nchi nyingi za Afrika bado hazijapa kipaumbele masuala ya usalama wa mtandao licha ya ushahidi unaoonyesha kuongezeka kwa mashambulio ya kimtandao yanayozidi kuwa ya hali ya juu.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *