Wizara ya Afya imethibitisha kupokea tetesi za uwepo wa ugonjwa wa Marburg katika Mkoa wa Kagera ambapo Wizara imepanga kutuma timu ya wataalamu kadhaa kuchukua sampuli kisha kufanyia uchunguzi Maabara.
Akithibitisha tetesi hizo Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama amesema ” Mpaka Januari 15, 2025 majibu ya uchunguzi wa kimaabara kutoka kwa wahisiwa wote waliochukuliwa sampuli hizo hayajathibitisha uwepo wa virus vya Marburg”
“Wizara inapenda kuwahakikishia wananchi pamoja na jumuiya ya kimataifa likiwemo shirika la Afya duniani (WHO) kuwa imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na itaendelea kutoka taarifa zaidi,”