Ewura yahimiza matumizi ya rasilimali ya joto ardhi kuzalisha umeme

Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeihimiza Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) kutumia vyema rasilimali ya jotoardhi kuzalisha umeme na kutekeleza kwa ukubwa shughuli nyingine za kiuchumi zitakazoongeza mapato ya kampuni hiyo na kuweka alama kwa taifa, kwa kuzingatia dhamana waliyopewa ya kusimamia rasilimali hiyo muhimu.

Akizungumza kwa niaba ya Bodi hiyo wakati wa kufunga ziara kwenye chanzo cha jotoardhi cha Songwe, Mjumbe wa Bodi, Fadhili Manongi alisema, “TGDC inapaswa kuhakikisha inaacha alama kwa taifa kwa kutumia rasilimali ya jotoardhi sio tu kuzalisha umeme, bali pia kuendeleza miradi mingine yenye tija iliyonayo ya utotoleshaji wa vifaranga, kilimo cha kisasa(greenhouse) na mabwawa ya kuogelea. Haya ni maeneo yanayoweza kuleta mapato zaidi kwa kampuni na maendeleo kwa jamii. Ni lazima juhudi ziongezwe kuhakikisha miradi hii inatekelezwa kwa kiwango kikubwa na kwa ufanisi.

Ziara ya Bodi ya EWURA, ambayo ililenga kufuatilia maendeleo ya miradi ya jotoardhi katika mikoa ya Mbeya na Songwe ili kuhakikisha inachangia kikamilifu katika upatikanaji wa nishati na ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *