Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Esther Mahawe amefariki dunia Januari 14, 2025 katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) Mkoani Kilimanjaro alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Hayo yamethibitishwa na msemaji wa familia ambaye anadai kuwa marehemu alikuwa anaugua kwa muda na walijitahidi kutaka kumsafirisha Dar es Salaam kwa matibabu lakini kutokana na hali yake kuwa mbaya madaktari wakashauri afikishwe kwanza KCMC.

Aidha Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Mohammed Mcherengwa kwa niaba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za rambirambi na kusema TAMISEMI pamoja na familia itashirikiana kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *