Rwegasha ateuliwa Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Umoja wa Afrika.

Mkurugenzi wa huduma za Tiba hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt. John Rwegasha ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Tiba, Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).

Dkt. Rwegasha amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa nafasi hiyo ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa katika mchakato wa usaili ambapo alikuwa na washindani kutoka mataifa saba Afrika.

Dkt. Rwegasha ni daktari bingwa mbobezi wa magonjwa ya mfumo wa chakula ini ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali Muhimbili.

Dkt. Rwegasha anatarajiwa kutumikia wadhifa wake mpya kuanzia Februari 2025.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *