Rais mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ameshiriki mkutano kuhusu uboreshaji wa kilimo barani Afrika kuelekea kupitishwa kwa programu ya kuendeleza kilimo Barani Afrika (CAADP 2026-2035) Kampala Jijini Uganda.
Kikwete ameshiriki mkutano huo akiwa kama mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Afrika na mjumbe wa bodi ya Shirika la Kimataifa la Muungano wa Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA).
Mkutano huo utafikia kilele kwa kupitishwa kwa azimio la Kampala na mkakati wa kihistoria wa miaka 10 na mpango kazi, ili kuimarisha uteketezaji wa Azimio la Malabo kuhusu ukuaji wa kasi wa kilimo na mabadiliko kwa ustawi wa pamoja na maisha bora lililopitishwa mwaka 2014.