Pato la mtanzania kufikia dola 4700

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo ametoa mwelekeo wa Taifa kupitia dira mpya ya maendeleo 2050, akisisitiza umuhimu wa kujenga Taifa jumuishi lenye ustawi, haki na linalojitegemea.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam leo Januari 13, 2025 katika mkutano wa kamati ya dini mbalimbali kuhakiki Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Profesa Kitila pia ameelezea mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya miaka 25 iliyopita.

“Tunahitimisha rasmi zoezi la kukusanya maoni ya uhakiki ya Rasimu ya Dira 2050. Tunakutana na taasisi za dini kwa sababu mnakusanya jamii kubwa ya Watanzania, na maoni yenu tunaamini yanaakisi maoni ya wengi,” amesema Profesa Kitila

Amesema tangu mwaka 2000 Tanzania imepiga hatua kwenye sekta mbalimbali ikiwamo elimu ambapo idadi ya wanafunzi wa shule za msingi wanaoendelea na sekondari iliongezeka kutoka chini ya asilimia 20 mwaka 2000 hadi asilimia 78 mwaka 2024, huku lengo likiwa ni kufikia asilimia 90 mwaka 2025.

Akizungumzia rasimu ya dira mpya Profsa Kitila amesema kuwa ifikapo mwaka 2050 Tanzania inalenga kuwa na uchumi wa kati wa hadhi ya juu, wenye pato la Taifa zaidi ya Dola Bilioni 500 za Kimarekani, kuongeza pato la mtu mmoja mmoja hadi kufikia zaidi ya Dola 4,700 kwa mwaka na kujenga uchumi jumuishi unaopunguza umasikini na kuongeza ustawi wa wananchi wote.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *