Bashungwa awataka wananchi kuchukua vitambulisho vyao vya NIDA.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Innocent Bashungwa amewataka wananchi kwenda kuchukua vitambulisho vyao vya taifa katika ofisi za Kata, Serikali za Mitaa, Vijiji na Shehia.

Alizungumza haya kwenye hafla ya uzinduzi wa mikakati ya mawasiliano ya Wizara, Vyombo vya Usalama vilivyopo chini yake na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika Ukumbi wa Suleiman Mzee uliopo Msalato Jijini Dodoma.

Waziri Bashungwa amesisitiza kuwa NIDA imefanya bidii kuzalisha vitambulisho kwa wananchi waliokuwa na namba za Utambulisho wa Taifa lakini hawakupata vitambulisho lakini hadi sasa vitambulisho vingi bado havijachukuliwa na wahusika.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *