Michuano ya FA imeendelea wikiendi hii ambapo kubwa zaidi ni klabu ya Arsenal kutolewa michuano hiyo dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Emirates.

Mchezo huo uliomalizika kwa sare ya 1-1 ulishuhudia Arsenal ikitolewa kwa mikwaju ya Penati (5-3) baada ya dakika 120 kumalizika.

Hali sio nzuri katika viunga vya Emirates na mashabiki wa Arsenal wameonekana kukata tamaa na kocha wao huku wengi wakiashiria aondoke.

Matokeo haya yameleta hisia tofauti juu ya klabu hiyo ikiwa ni siku chache kabla kukubali kipigo cha 2-0 nyumbani dhidi ya Newcastle katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Carabao.

Mbali na matokeo hayo huenda Arsenal wakamkosa mshambuliaji Gabriel Jesus ambaye atakuwa nje kwa kipindi kisichofahamika baada ya kupata majeraha ya goti.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *